Mwakilishi wa Viti maalum Mkoa wa Magharibi kichama,  Mhe. Mwanaidi Kassim Mussa akizungumza wakati akikabidhi vifaa vya ujenzi ikiwemo saruji na matofali kwa Wana CCM wa Tawi la Nyamanzi na Wadi ya Pangawe katika Wilaya ya Dimani kichama. 

Na Takdir Ali. Maelezo. 

Mwakilishi wa Viti maalum Mkoa wa Magharibi kichama Mhe. Mwanaidi Kassim Mussa amewataka Wazazi na Walezi kushirikiana katika kuwakinga Wataoto wao na atahari za Utandawazi.

Ameyasema hayo kwa nyakati tofauti mara baada ya kukabidhi vifaa vya ujenzi ikiwemo Saruji na matofali kwa Wana CCM wa Tawi la Nyamanzi na Wadi ya Pangawe katika Wilaya ya Dimani kichama.

Amesema baadhi ya Watoto wanatumia vibaya mitandao ya kijamii vibaya kwa kuangalia Ngono jambo ambalo linapelekea kuiga vitendo kwa kufanya vitendo viovu.

“Watoto wetu wakiona mambo katika mitandao hawakubali wanaenda kuyafanyia kazi, lazima Wazazi wenzangu tuwambie Watoto wetu tusiwaogope, maana wakati huu tunawaogopa Watoto wetu hata kuwaambia jambo lolote”alisema Mwakilishi Mhe. Mwanaidi.

Hata hivyo amewataka kubadilika na kurudisha malezi ya zamani ya kukaa na Watoto wao ili kuweza kuwakinga Watoto wao na vitendo viovu ikiwemo Udhalilishaji, Ukatili na Utumiaji wa Dawa za kulevya.

Aidha Mhe. Mwanaid amempongeza Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dk. Samia Suluhu Hassan na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi kwa kuwatumikia Wananchi na kuvuuka lengo katika kutekeleza Ilani ya Chama Cha Mapinduzi ya mwaka 2020-2025 kwa vitendo. 

Mbali na hayo amewasisistiza kuwa na Umoja, Upendo na Mshikamano miongoni mwao ili waendelee kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi ikiwemo kuhamasisha vijana wenye sifa kushiriki katika Uandikishaji wa Daftari la kudumu la wapiga kura wakati utakapofika.

Kwa upande wake Katibu wa UWT Wilaya ya Dimani kichama Saada Juma Ramadhani amesema lengo la kukabidhi msaada huo ni Mhe. Mwanaidi kuteleleza ahadi alioiweka katika Tawi hilo.

Aidha amesema Wanaccm wa Tawi hilo kuitumia fursa ya kuanzisha miradi mbalimbali ya maendeleo kama vile masomo ya ziada ili iweze kuwasaidia Watoto wao kupata elimu.

Nao Wana CCM wa Tawi la Nyamanzi na Wadi ya Pangawe Wilaya ya Dimani kichama wamempongeza Mwakilishi huyo kwa kukabidhi vifaa hivyo vya ujenzi ikiwemo Saruji na Matofali wameahidi kuvifanyia kazi ili  kufikia malengo yaliokuwa.


 Mwakilishi wa Viti maalum Mkoa wa Magharibi kichama,  Mhe. Mwanaidi Kassim Mussa akikabidhi vifaa hivyo vya ujenzi.